Mbeya ‘Cement’ yarudisha fadhila kwa wananchi
10 November 2023, 14:03
Mwandishi Samweli mpogole
Kampuni ya Saruji (Mbeya Cement Ltd) imetoa hekari 700 kwa wanakijiji wa Songwe Viwandani halmashauri ya wilaya ya Mbeya Kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo
Hatua hiyo ni sehemu ya mchango wa uwekezaji Kwa wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za kilimo jirani na kampuni hiyo ya Saruji
Akizungumza na Highlands Fm Radio, Katibu wa Kampuni ya Saruji (Mbeya) Ian Almachius amesema wakiwa wadau wa uwekezaji kipaumbele Chao ni kushirikiana na jamii inayowazunguka
“Kwa kawaida tumekuwa tukishirikiana na serikali za vijiji, Hadi sasa tumetoa hekari 700 Kwa ajili ya kilimo, lakini tumepokea jumla ya maombi 160, hivyo tunatoa wito Kwa mwanakijiji yoyote ambaye hajaelewa utaratibu aje aulize kwetu au Kwa viongozi wa serikali”
AsemaAwali kuliibuka sintofahamu ya kuyatumia mashamba ya kampuni hiyo kufuatia baadhi ya watu kuyakodisha Kwa wananchi kinyume na utaratibu au kujimilikisha Kwa muda mrefu bila kufuata miongozo ya uendeshaji wa ardhi hiyo
Akitolea ufafanuzi suala hiyo, Ian amesema kampuni ina miongozo yake na lazima ifuatwe ikiwemo kuwatambua wananchi wanaofanya shughuli za uzalishaji kwenye ardhi hiyo.Diwani wa kata ya Bonde la Songwe Michael Ngailo amesema wanatumia mikutano ya hadhara kuwaelimisha wananchi kunufaika na fursa hiyo Kwa kufuata utaratibu mzuri
“tunaendelea kusimamia ugawaji wa mashamba hayo kwa kutoa elimu kwa wananchi pia kuwagawia kutokana na makubaliano yaliyopo kati ya serikali na kampuni ili wananchi wa eneo letu wanufaike Moja kwa moja”.