CCM Mbeya yamtambulisha katibu mwenezi mpya
4 November 2023, 17:26
Mwandishi : samweli ndoni
Chama Cha Mapiduzi (CCM) mkoa wa Mbeya kimemtambulisha katibu wa siasa na uenezi wa Chama hicho ngazi ya mkoa Christopher Uhagile, akichukua nafasi ya Bashiru Madodi ambaye amepangiwa majukumu mengine ya kichama.
Akimtambulisha kwa waandishi wa habari, Mjumbe wa halmashauri kuu taifa (NEC), Ndele Mwaselela amesema Uhagile amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bashiru Madodi ambaye ameteuliwa kuwa katibu wa CCM, wilaya ya Mbinga.
Amesema kwa niaba ya chama anaamini kiongozi huyo anakwenda kutekeleza majukumu yake vyema kwa kuwa wanafahamu utendaji kazi wake tangu wakati akiwa anatumikia nafasi nyingine ndani ya Chama.
“Kwa mujibu wa katiba ya CCM, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa ndiye anakuwa msimamizi wa vikao endapo nafasi hiyo itakuwa wazi, hivyo kwa sababu mwenyekiti wetu amepangiwa majukumu mengine mii ndiye nasimamia vikao vyote ngazi ya mkoa, hivyo ninamtangaza Christopher Uhagile kuwa katibu mwenezi wa chama mkoa wetu wa Mbeya’’
Naye katibu mwenezi mpya aliyeteuliwa Christopher Uhagile, amesema jukumu kubwa alilokuwa nalo ni kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM kwa wananchi