RC Homera ataka wahitimu TIA kuwa na nidhamu ya fedha
3 November 2023, 20:25
na ,Prince Fungo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka wahitimu wa taasisi ya fedha ya uhasibu (TIA) kampasi ya Mbeya kutumia maarifa waliyoyapata chuoni hapo Kwenda kutatua changamoto za kiuchumi kwenye jamii ikiwemo kuwa na nidhamu ya fedha kwenye matumizi yao ya kila siku ili kuwa na kipato stahimilivu.
Akizungumza kwenye mahafali ya kumi na moja ya taasisi hiyo kampasi ya Mbeya homera ameipongeza taasisi hiyo kwa kuwaanda wataalamu mahili wa masuala ya usimamizi wa fedha ambao wamejizolea sifa kupitia taasisi na sekta mbalimbali ambazo wanazisimamia
Homera ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo amewakumbusha wahitimu Kwenda kutumia maarifa walio yapata chuoni kuimarisha kipato chao na taifa kwa ujumla kw akua na nidhamu ya fedha na kupangilia bajati kwenye matumizi yao.
kwa upande wake mjumbe wa bodi ya ushauri wa wizara ya fedha Emma Lyimo amesema miongoni mwa mkakati uliopo ni kuhakikisha wahitimu wa taasisi hiyo wanakwenda kutumia utaaluma walioupata kuchangia shughuli za kiuchumi kupitia kwa wajasiriamali wadogo.
Naye mhitimu wa chuo hicho, Leah Mbedule amesema maarifa aliyopata yamemuandaa kikamilifu kwenye stadi za Maisha ya kujitegemea, akieleza hadi anafikia hatua ya kuhitimu tayari anamiliki miradi yake ikiwemo ufugaji wa kuku Pamoja na kilimo cha viazi.