Wananchi wa ilembo halmashauri ya wilaya ya mbeya waondokana na adha ya umeme
9 October 2023, 13:39
Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo elimu ambapo wanafunzi wamekuwa wakipata elimu na kutimiza ndoto zao
Na Samweli Mpogole
Wananchi wa Kata ya Ilembo Halmashauri ya Wilaya Mbeya wameishukuru Serikali kwa Kuwafikishia huduma ya Umeme pia kuwajengea Sekondari ya Wasichana ya Pareto
Shukrani hizo zimetolewa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa alipo tembelea Katika kata hiyo Ili kuona Maendeleo ya ujenzi wa shule ya wasichana Pareto na kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo ambapo Wananchi waliibuka na kutoa hisia zao Juu ya kile kilichofanywa na Serikali l.
Hata hivyo wameendelea kusema kuwa Serikali imefanya jambo muhimu kuwashirikisha wadau Ili kusaidia Ujenzi wa Shule ya wasichana itakayosaidia wasichana waliopo katika kata hiyo kutotembea umbali mrefu kufuta huduma ya elimu
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya amesisitiza Wakazi wa Ilembo na Halmashauri ya Wilaya Mbeya kushirikiana ipasavyo na Makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao la Pareto ambao waliahidi Kuchangia Katika ujenzi wa Shule hiyo haraka iwezekanavyo.
Aidha Malisa amewasisitiza Wakazi wa Ilembo kuwa wavumilivu Kwakuwa Serikali yao ni Sikivu na itendelea kuwapelekea maendeleo katika maeneo hayo ikiwemo kuboresha Miundombinu ya Barabara na Maji.