Vibaka watoto tishio Ndobo Kyela
26 September 2023, 16:20
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanafunzi wilayani Kyela kujiingiza katika vitendo viovu na kupelekea kushindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali na wengine kujiingiza katika wimbi la uhalifu.
Na Samwel Mpogole..
Imeibuka tabia kwa baadhi ya vijana katika kata ya Ndobo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kukataa kuendelea na masomo na kujihusisha na vitendo vya wizi, hali ambayo imekuwa tishio na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.
Wakazi wa kata hiyo wametoa malalamiko hayo kwenye mkutano ulioandaliwa na mbunge wa jimbo la Kyela Mheshimiwa Ally Mlagila kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Sauti za wananchi
Baada ya wananchi kutoa malalamiko hayo mkuu wa polisi wilaya ya Kyela, Lwitiko Mwanjala ametoa onyo Kali kwa vibaka sambamba na kuwataka waache maramoja tabia hizo
Mkuu wa polisi ya kyela Lwitiko Mwanjala
kwaupande wake Mbunge huyo wa Jimbo hilo amesikitishwa na vitendo hivyo viovu vinavyo lalamikiwa na wananchi wa eneo Hilo huku akiwataka viongozi kuhakikisha wanashughulikia kikamilifu malalamiko yote yaliyo bainika.
Mbunge wa jimbo hilo Ally Mlagila