Wananchi waishio mpakani waomba elimu zaidi chanjo ya polio
25 September 2023, 17:52
Baadhi ya wananchi waishio mipakani mwa Tanzania na Malawi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya chanjo ya polio kwani baadhi yao wameshindwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo.
Na Samwel Mpogole
Wananchi waishio mpakani mwa Tanzania na Malawi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu sambamba na utoaji wa chanjo ya polio kwani baadhi yao bado hawajafikiwa.
Wakiongea na kituo hiki kwa nyakati tofauti wananchi hao wameishukuru serikali kwa kuhakikisha inawafikia ambapo pia wametumia nafasi hiyo kuomba muda wa utolewaji chanjo uongezwe kwani kuna baadhi yao walikuwa mbali na maeneo yao ya makazi.
Chanjo ya polio ilianza kutolewa 21 September hadi 24 September kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 katika mikoa 6 ambayo inapakana na nchi zenye mlipuko wa polio ambyo ni Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi,, Songwe na Mbeya.