Viongozi wa dini wajitosa kuokoa ndoa
22 September 2023, 13:10
Unapoingia katika ndoa au mahusiano huwezi kufikiria hata kidogo kwamba asilimia kubwa ya ndoa au mahusiano hayo kufeli, ndoa au mahusiano yanaweza kufeli kwa sababu nyingi na iwapo ndoa yako ilianguka na kufeli sababu kubwa yaweza kuwa na tofauti nyingine.
Na Samweli Mpogole
Viongozi wa dini wametakiwa kuhakikisha wanatoa elimu ya ndoa na malezi kwenye nyumba za ibada ili kuepuka vitendo vya ukatili vinavyoendelea kwenye jamii.
Wito huo umetolewa na Askofu Profesa Donald Mwanjoka Mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG ICC, Mbeya alipokuwa akizungumza na Highlands Fm Radio.
Mwanjoka amesema kuwa ni jukumu la viongozi wote waliopo katika nyumba za ibada kuhakikisha wanatoa elimu na mafunzo sambamba na kutenga madarasa kwa makundi rika na jinsia ili kutoa elimu ya kina kuepuka jinamizi linalo ikabili jamii juu ya ukatili.
Aidha Askofu huyo amewaasa wanaume kuwa karibu zaidi na Mungu kwani wao ni waganga zaidi hivyo wakiwa karibu na Mungu kwakufika katika nyumba za ibada itawasaidia kuepukana na vitendo hivyo.