Wanahabari wapewa mafunzo ya habari za afya kuibua yaliyojificha kwenye sekta ya afya
20 September 2023, 14:14
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii ESRF Tanzania inaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa Radio Jamii nchini ili kusaidia katika juhudi za kuboresha huduma za afya katika jamii
na isack mwashiuya
Mafunzo hayo ya siku 4 yameanza rasmi tarehe 19 Septemba 2023 katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam yakiwashirikisha watangazaji na waandishi wa habari takribani 47 kutoka radio mbalimbali za kijamii ikiwamo radio Highlandsfm radio
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa ESRF, Prof Fortunata Songora Makene amesema mafunzo hayo yameandaliwa kama sehemu ya mradi wa Utafiti ujulikanao kwa jina la ‘Afya Yako’ ambao umelenga katika tafiti ya maeneo makubwa mawili.
Akiyataja maeneo hayo prof Makene amesema ni kugundua nafasi ya Redio za jamii katika kupambana na taarifa potofu za afya ya jamii na eneo la pili ni kubaini nafasi ya mwandishi wa habari za uchunguzi katika uboreshaji wa utoaji wa huduma za afya nchini hususani katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya.