Akina baba wanyooshewa kidole kutoshiriki kikamilifu malezi ya watoto
15 September 2023, 19:35
Na Mwandishi wetu Isack Mwashiuya
Imebainika kuwa ‘ubize’ wa wazazi na ushiriki mdogo kwa akina baba katika malezi ya mtoto tangu anapozaliwa ni moja kati ya sababu ya watoto wengi kuwa na uwezo mdogo wa uelewa na kuwa wazito katika kuchakata baadhi ya mambo pindi wanapokua.
Hayo yanajiri wakati ambao wataalam wa afya wakibainisha kuwa ubongo wa mtoto hukua kwa haraka zaidi kuanzia anapokuwa na miaka 0-3 hivyo wazazi wameshauriwa kuzingatia zaidi suala la malezi ili kumjengea mtoto uelewa na uwezo mkubwa wa kufikiri.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Benno Malisa ambaye pia ni mgeni rasmi katika kikao kazi na viongozi wa kata 36 jijini Mbeya katika kuhamasisha mpango wa taifa wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kilichoratibiwa na taasisi binafsi ya WE CARE FOUNDATION kwa kushirikiana na HELVETAL taasisi zinazijihusisha na malezi , makuzi na maendeleo bora ya mtoto kilichoketi katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Benno Malisa
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa WE CARE FOUNDATION Elica Thobias amefafanua sababu, maono na mpango wa taasisi yake kwa wakazi wa Mbeya na maeneo jirani juu ya malezi kwa watoto.
Mkurugenzi Mtendaji Elica Thobias
Nao baadhi ya akina baba walioshiriki kikao hicho wamefafanua namna ambavyo wanaelewa na walichojifunza juu ya umuhimu wa baba kushiriki katika makuzi ya mtoto.
Sauti za akina baba
Kwa upande wao madiwani wakiwakilishwa na diwani wa kata ya Maendeleo Issa Shabani wamepongeza wazo la wadau pamoja na serikali katika kujenga kizazi chenye afya.
Diwani kata ya maendeleo Issa Shabani
Licha ya serikali kuwa na mpango wa kuanzisha vituo vya malezi katika maeneo maalum ikiwemo kwenye masoko makubwa imeelezwa kuwa akina baba wana nafasi kubwa katika kufanikisha makuzi bora kwa mtoto…