Halmashauri ya wilaya ya chunya yavuka kiwango cha mapato ya ndani
12 September 2023, 11:14
Makusanyo hayo yanaifanya halmashauri hiyo kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ambalo lilikuwa ni sh. Bilioni 27.9 katika kipindi cha mwaka 2022/2023
Na Samwel Mpogole
Zaidi ya shilingi bilioni 29.8 zimekusanywa kama mapato ya ndani na halmashauri ya wilaya ya Chunya katika kipidi cha mwaka wa fedha 2022/23.
Akitoa taarifa kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Chunya,mwenyekiti wa baraza hilo Bosco Mwanginde amesema kutokana na makusanyo hayo halmashauri imevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 106.
Kwa upandewake Venance Luwagila Afisa uhamiaji wilaya ya chunya ameliomba baraza hilo kutoa elimu kwenye jamii kuhusu elimu ya kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu
Aidha Lutufyo Mwambungu, Mkuu takukuru wilaya ya chunya, amewasihi madiwani hao kuwa na ushirikiano sambamba na kukagua miradi kwakuwa jamii inaamini kupitia wao hivyo kuto kukagua miradi kunaweza iletea hasara serikali
Katika hatua nyingine Anakleth Michombero Katibu tawala, akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya chunya amewapongeza madiwani hao kwakutokuwa miongoni mwa halmashauri tano zilizo kwenye sakata la ubadhilifu wa fedha za uma kupitia mashine za ukusanyaji mapato ambapo amewataka kuendelea kusimamia kwa umakini fedha na miradi katika maeneo yao.
Kwaupandewake Eliah Chigoji akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera, amewataka madiwani hao kuhakikisha wanaongeza vyanzo vingine vya mapato ili kuendelea kufanya vizuri zaidi
Katika kikao hicho madiwani wameadhimia kurejea katika nafasi ya kwanza kuongoza ukusanyaji mapato katika mkoa wa mbeya sambamba na kuendelea kuvuka lengo kila awamu ili kuwa mfano wa kuigwa katika halmashauri nyingine.