Mkoani FM

Recent posts

17 September 2023, 4:47 pm

70% ya wakulima hulima kilimo cha mazoea Pemba-Utafiti

Imeelezwa kuwa wakulima kisiwani Pemba bado wanalima kilimo cha mazoea ambacho hawazingatii  maelekezo ya kitaalam juu ya kilimo jambo ambalo linapelekea kukosa mavuno mazuri hasa wale wanaolima kibiashara. Na Khadija Yussuf Wakulima kisiwani Pemba wametakiwa kuacha tabia ya kulima kimazoea…

14 September 2023, 4:53 pm

ZEC kutoa  tarehe ya uchaguzi mdogo Mtambwe

Kufuatia kifo cha aliyekuwa  Mwakilishi wa jimbo la mtambwe Habibu Ali Mohamed, tume ya uchaguzi  Zanzibar imeamua kufanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi hiyo iliopo wazi na wadau wote wa uchaguzi wanatakiwa kushiriki kukamilisha uchaguzi huo kama ilivyokusudiwa. TUME ya Uchaguzi…

14 September 2023, 3:58 pm

Vipindi  vya elimu Redioni vitaengeza ufaulu Sekondari.

Vipindi vya elimu vya redio zinasaidia kuengeza ufauli kwa wanafunzi hasa wa sekondari ni vyema wazazi na walimu kushirikiana kwa pamoja kuwahimiza watoto wao  kufuatilia vipindi hivyo kwa lengo la kuengeza ufaulu. Na Fatma Rashid. Meneja wa mradi wa  Secondary …

12 September 2023, 9:23 pm

Makoongwe waomba huduma bora za kijamii

Wananchi wa kisiwa cha Makoongwe kinachopatikana mkoa wa Kaskazini Pemba wameomba kupatiwa huduma mbalimbali za kijamii kutokana na huduma hizo kukosekana muda mrefu na kumtaka mbunge wa jimbo la Mkoani kutimiza wajibu wake kwao. Na Khatib Juma Wananchi wa shehia…

9 September 2023, 1:37 pm

Idara ya Tiba Pemba: Endeleeni kutumia vyandarua kumaliza ugonjwa wa malaria

Ugonjwa wa malaria bado upo visiwani Zanziabr hivyo jamii inatakiwa kutumia vyandarua vinavyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya kitengo cha malaria kwa kushirikiana na  wahisani  mbalimbali wa maendeleo  kwa ajili ya kujifunika na sio kuvifunga kwenye bustani za bogaboga …

8 September 2023, 12:56 pm

Kamati za kupinga ukatili Zanzibar zatoa neno kupunguza talaka

Visiwani Zanziabar kumekuwa na engezeko la talaka kila siku hali hiyo ndio imepelekea  kamati maalum ya kupinga  vitendo vya udhalilishaji  Zanzibar kutoa ushauri kwa serikali kwa kutoa elimu hiyo skuli na madrsa. Na Mwandishi wetu. Kamati za kupinga vitendo vya…

8 September 2023, 12:02 pm

Mtu mmoja ajeruhiwa na watu wasiojuilikana Pemba

Mmiliki wa kambi ya uchumaji  zao la karafuu anajeruhia na watu wasiojuuilikana huko kambini kwake  matukio hayo yanajitokeza kila msimu wa karafuu unapofika  kisiwani Pemba. Na Mwandishi wetu. WATU wasiofahamika Wadaiwa kuvamia kambi ya karafuu na Kumshambulia kwa vitu vyenye…

Mkoani Fm

Kiswahili

      Radio Jamii Mkoani ni taasisi isio ya kiserekali na isilo na lengo la kugawana faida. Taasisi hii ilianzishwa kwa makubaliano ya pamoja ya wanajamii wa Wilaya ya Mkoani kua ni kituo cha Radio ambacho kitarusha matangazo yake kwa mustakbali wa maendeleo ya jamii.

Kituo hichi kilifungiliwa rasmi tarehe 03/01/2015 na kusajiliwa rasmi mnamo 13/06/2016 nakupewa lesi ya utangazaji na Tume ya Utangazaji Zanzibar (Zanzibar Broadcasting Commission) chini ya sheria ya mwaka 2003 kifungu 12 (1) cha huduma za utangazaji.

Lengo kuu la kunzishwa taasisi hii ni kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu na kupunguza matatizo mbali mbali yanayorudisha nyuma maendeleo ya jamii katika Wilaya ya Mkoani na maeneo mengine ya karibu kupitia programu mbali mbali za Radio na mitandao ya kijamii.

Kituo hichi kina wataalamu mbali mbali waliobobea katika kuandaa na kurusha programu na vipindi mbali mbali vinavyotoa mwamko wa maendeleo na kupunguza matatizo yanayoikumba jamii zetu. Hadi kufikia sasa, Kituo hichi kimejijengea sifa za kutosha katika kipengele cha kuelimisha jamii kupitia program zilizoandaliwa kwa umakini mkubwa kikishirikiana na taasisi mbali mbali.

Radio jamii imefanikiwa kuendesha program za kupambana na ubaguzi wa kijinsia, ndoa za utotoni, kutumikishwa kwa watoto, migogoro ya kijamii, malezi mabovu, vitendo vya ukatili, ubakaji, wizi wakupindukia, tabia mbovu, madawa ya kulevya, miripuko ya maradhi mbali mbali, uharibifu wa mazingira nk. Pia, imehamasisha mambo mbali mbali mazururi ikiwemo ubunifu wa ajira kwa vijana, kutafuta elimu, uzalishaji mali, stadi za maisha, kutoa elimu ya uraiya na kuhamasisha wanawake kushiriki kwenye nafasi za uongozi.

DIRA

Kuwa chombo imara cha kuunganisha jamii kuwa moja iliyoelimika yenye afya na uchumi imara

DHAMIRA

Kukuza Maendeleo ya Wilaya ya Mkoani Kiuchumi, Kielimu, Kiafya na kuanzisha Jukwaa la mjadala wa kuleta Maendeleo ya Wilaya.

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

English

Mkoani Community Radio is not for profits, it is a non governmental Organization established by nationalists from Mkoani District in 2015  and was official registered  under the society Act No.6 of 1995 of Zanzibar Revolutionary Government for the purpose of contributing in national and global efforts of bring about sustainable  development and poverty reduction in the community by  providing community radio broadcasting services  at Mkoani areas and adjacent locales.

The Radio contributes to the social economic and political wealth of our local community in Mkoani areas and adjacent setting by providing access to a truly independent, community owned and run local radio station. It has professional and experienced personnel on local and National level Radio broadcasting program. It works through its already established structures led by Executive committee that  is responsible for day –to day management of the station which include planning ,implementation and monitoring of the activities.

VISSION

To be a strong institution this will build a united community, educated and economical wel being.

MISSION

To enhance the development of Mkoani district economically, educationally and good health condition. to develop a fourm to discuss and bring Mkoani district in a sustainable Development.