Highlands FM

FCC kula sahani moja na wasambazaji bidhaa bandia

27 May 2024, 18:00

Mkuu wa kanda Nyanda za Juu Kusini Tume ya Ushindani {FCC} Dickson Mbanga akitoa elimu kwa wananchi namna ya kutambua bidhaa bandia.

Na Lameck Charles

Elimu hiyo inayotolewa kwenye maonesho ya Mbeya Expo 2024 yanayoendelea kufanyika jijini Mbeya  imehusisha wafanya Biashara wadogo,wakati na wakubwa Kwa lengo la kunufaika na fursa mbalimbali za Biashara.

Dickson Mbanga ni Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (FCC) amesema lengo la FCC ni Kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi Ili wawe na uelewa kuhusu Haki zao kama walaji.

Katika kipindi Hiki Cha maonesho ya Mbeya Expo 2024 Fcc itaendelea kutoa Elimu hivyo ni fursa Kwa Wananchi kufika na kujifunza na kupata uelewa kuhusu bidhaa Bandia,kueleza malalamiko yao nk.

Maonesho ya Mbeya Expo yanayoratibiwa na Chemba ya wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya TCCIA yanaendelea kufanyika Kwenye viwanjaa wa Uhindini Jiji Mbeya Hadi May,30,2024.

Baadhi ya wanafunzi wakipatiwa mafunzo katika banda ya maonyesho la FCC ndanya za juu kusini.