Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
31 October 2026, 8:07 am

“Uchumi wa Mkoa wa Mara kwa kiasi kikubwa unategemea sekta za ufugaji, utalii (wanyamapori) na uvuvi na uchafu ukikithiri hususan kwa kutupa ovyo taka za plastiki unahatarisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla” Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi
Na Amos Marwa
Mkuu wa Mkoa wa Mara Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi amekabidhi tuzo za usafi za miezi ya Septemba na Oktoba, 2026 kwa Halmashauri zilizofanya vizuri na kinyago kwa Halmashauri iliyofanya vibaya zaidi kwenye usimamizi wa usafi katika Mkoa wa Mara.
Akizungumza katika utoaji wa tuzo hizo, Mtambi amesema Mkoa wa Mara hautavumilia uchafu wa mazingira kwa kuwa uchafu na kuwataka wilaya ya Serengeti mshindi wa kwanza, ikifuatiwa na Manispaa ya Musoma na halmashauri ya Mji wa Tarime waliofanya vizuri wasibweteke kwani zoezi hilo litakuwa endelevu na litafanyika kila mwezi

Mtambi amesema mashindano hayo ni endelevu na kuanzia sasa yatafanyika kila mwezi ili kulinda afya na uchumi wa wananchi na uchumi wa Mkoa kwa kuhakikisha kuwa suala la usafi wa mazingira linakuwa endelevu.

Katika mashindano ya usafi, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imekuwa mshindi wa kwanza, ikifuatiwa na Manispaa ya Musoma na Halmashauri ya Mji wa Tarime ambazo zimepewa tuzo na hati ya pongezi wakati Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ikishika nafasi ya mwisho na kukabidhiwa kinyago.
