Butiama FM Radio

Mara kuchanja mifugo zaidi ya milioni 3.5 katika awamu ya pili ya kampeni ya chanjo

18 November 2026, 10:24 am

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi, akizungumza na wandishi wa habari wakati ofisini kwake wakati wa kuzindua awamu ya pili ya kampeni ya chanjo ya mifugo mkoa wa Mara.Picha na Gabon Mariba

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi, amezindua awamu ya pili ya kampeni ya chanjo ya mifugo, inayolenga kuchanja mifugo 3,576,019 wakiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku.

Na Gabon Mariba

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi, amezindua awamu ya pili ya kampeni ya chanjo ya mifugo, inayolenga kuchanja mifugo 3,576,019 wakiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Novemba 12, 2026, Mtambi amesema maandalizi yote yamekamilika na zoezi hilo limeanza katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mara.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi

Mtambi amesema kampeni hiyo inalenga kulinda afya ya mifugo, kuzuia milipuko ya magonjwa, kupunguza vifo vya mifugo na kuongeza uzalishaji ili kuinua tija na kipato cha wafugaji.

Aidha, amesema kampeni hiyo inalenga kuiwezesha mifugo na mazao yake kukidhi viwango vya kimataifa ili kuongeza fursa ya kuingia katika masoko ya kimataifa.

Amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia Halmashauri katika utekelezaji wa kampeni hiyo ili wafugaji wapate huduma za chanjo na utambuzi wa mifugo katika maeneo yaliyotengwa kwenye vijiji na mitaa bila usumbufu.