Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
26 October 2026, 8:04 am

Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza mauaji ya Manka, mfanyakazi wa nyumba ya kulala wageni huko Butiama, mkoani Mara, ambaye mwili wake umekutwa umefichwa chini ya kitanda ndani ya chumba cha gesti hiyo.
Na Oscar Mwakipesile
Mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Manka, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25, mkazi wa Moshi, mkoani Kilimanjaro, ameuawa na watu wasiojulikana katika nyumba ya kulala wageni iliyopo kijiji cha Butiama, wilayani Butiama. Mwili wake umekutwa ukiwa umefichwa chini ya kitanda ndani ya moja ya vyumba vya nyumba hiyo, Manka alikuwa mfanyakazi katika nyumba hiyo ya kulala wageni kabla ya kukumbwa na mauti hayo.
Akizungumza na Butiama FM, mmiliki wa nyumba hiyo, Magembe Wanzagi, amesema tukio hilo liligundulika baada ya mwanamke mwingine ambaye ni mpishi katika eneo hilo kubaini kutokuwepo kwa Manka, na juhudi za kumtafuta zilipoanza, ndipo mwili wake ulipokutwa ndani ya chumba kimoja katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
Jeshi la Polisi limedhibitisha kutokea kwa mauaji hayo katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu ili kubaini chanzo cha kifo chake. Polisi wamesema kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea, na kwamba taarifa zaidi kuhusu mazingira ya mauaji hayo zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
