Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
18 November 2026, 11:25 am

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Thecla Mkuchika, amewataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama mara moja na kwenda maeneo salama kujikinga na athari za mvua kubwa, huku akiwataka madiwani kuimarisha utoaji wa elimu ya tahadhari na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Na Amos Marwa
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Thecla Mkuchika, amewaonya wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni kuhama mara moja na kwenda maeneo salama ili kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza wakati wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Mkuchika amewataka madiwani kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari ya mvua za El Nino zilizotangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Aidha, amesisitiza umuhimu wa wananchi kuzingatia tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika na kuepuka kuishi au kuendelea na shughuli katika maeneo hatarishi wakati huu wa mvua.
