Butiama FM Radio

Jamii Butiama yapewa Elimu kuhusu uhalifu

18 April 2026, 11:20 am

Mkuu wa oparesheni wilaya ya Butiama Asp Laban Akeyo akizungumza katika kipindi maalumu cha jeshi la polisi kutoa elimu kwa jamii kinachoruka kila siku ya Alhamis akielezea aina na jinsi ya jamii kuweza kupambana na uhalifu. Picha na Amos Marwa.

Kuna aina nyingi za uhalifu ikiwemo uhalifu dhidi ya mali, uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu dhidi ya maadili ya jamii yetu  na uhalifu wa kimtandao hizo zote zinasumbua jamii.

Na Oscar Mwakipesile

Jamii Wilaya ya Butiama imepewa elimu kuhusu uhalifu na namna nzuri ya kukabiliana na uhalifu katika jamii ili  kwendeleza amani katika jamii.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa opareshioni wilaya ya Butiama Asp Laban Akeyo alipozungumza kupitia Butiama FM katika kipindi maalumu   na kusema kuwa ukosefu wa ajira na  vijana kutamani kuwa na maisha mazuri kwa kuiga maisha mitandaoni kumechochea kuongezeka Kwa uhalifu katika jamii na kuelezea viashiria mbalimbali ambavyo wananchi wanaweza kuvitambua ili Kupunguza uhalifu huku akielezea aina mbalimbali za uhalifu.