Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
28 April 2026, 2:20 pm

”Wananchi wanapaswa kuthibitisha habari kupitia vyanzo rasmi na vyakuaminika kama Butiama FM kabla ya kusambaza habari hiyo lakini pia kuepuka kusambaza maudhui yasio na staha kwa jamii yetu” ASP Ponsian Kalinjuma, mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Butiama,
Na Oscar Mwakipesile
Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Butiama, ASP Ponsian Kalinjuma, ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuepuka kuathirika na vitendo vya uhalifu vinavyozidi kuongezeka. Akizungumza katika kipindi maalum cha redio cha Butiama FM, amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia majukwaa hayo kueneza taarifa za upotoshaji, kufanya utapeli pamoja na kuvuruga amani ya jamii.
ASP Kalinjuma amesisitiza umuhimu wa wananchi kuhakiki vyanzo vya taarifa wanazopokea kabla ya kuzisambaza kwa wengine, akibainisha kuwa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ni silaha muhimu ya kupambana na uhalifu huo. Aidha, amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapobaini viashiria vya uhalifu mtandaoni, ili kulinda usalama na ustawi wa jamii kwa ujumla.