Butiama FM Radio

Mila kandamizi zachochea ukatili wa kijinsia Butiama

27 April 2026, 3:24 pm

Sajenti Haruna Ramadhani Mtoy kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Butiama, akielezea baadhi ya mila na tamaduni zinazoeweza kusababisha ukatili katika jamii, kupitia kipindi maalumu kinachoruka jumamosi asubuhi na Butiama FM. picha na Amos Marwa

Ukiozesha mtoto mdogo ambaye hajafikia umri sahihi hilo ni kosa la jinai mzazi atachukuliwa hatua kwa mujbu wa sheria kuna baadhi ya wazazi wanasema mtoto mwenyewe karidhia hiyo haikubaliki mtoto hana maamuzi ya kuingia kwenye ndoa kabla ya muda” Sajenti Haruna Ramadhani Mtoy kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Butiama.

Na Amos Marwa

Katika jitihada za kuelimisha jamii kuhusu haki za binadamu, Sajenti Haruna Ramadhani Mtoy kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Butiama ameeleza kuwa baadhi ya mila na tamaduni zimekuwa chanzo kikubwa cha vitendo vya ukatili katika jamii, akizungumza katika kipindi maalumu kupitia Butiama FM , Sajenti Mtoy amebainisha vitendo kama ukeketaji, kurithi wajane bila ridhaa, pamoja na kuwanyima watoto wa kike haki ya urithi kuwa vinaathiri ustawi wa wanawake na watoto.

Amesisitiza umuhimu wa jamii kubadili mtazamo na kuachana na mila hizo kandamizi, huku akihimiza wazazi na walezi kutoa elimu sahihi kwa watoto na kushirikiana na mamlaka husika kupambana na vitendo vya ukatili. Aidha, ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa mapema wanaposhuhudia ukatili ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.