Butiama FM Radio

Butiama yaweka mkazo usafi wa mazingira

21 June 2026, 7:46 am

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Thecla Mkuchika, akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa kampeni ya usafi wa mazingira ya kila Jumamosi ijulikanayo kama “Ondoa Taka Butiama” uliofanyika kata ya Butiama. Picha na Absalom Tweve

Hakuna mfanyabiashara anayepaswa kupuuza kampeni hii ya usafi. Wale ambao hawakuhudhuria leo, majina yao yaandikwe kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria, Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Thecla Mkuchika.

Na Amos Marwa

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Thecla Mkuchika, amezindua rasmi kampeni ya usafi wa mazingira ya kila Jumamosi ijulikanayo kama “Ondoa Taka Butiama”, akisema hatua hiyo inalenga kujenga utamaduni endelevu wa usafi na kuhakikisha mazingira ya wilaya hiyo yanakuwa salama na yenye afya kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Kijiji cha Butiama, Mkuchika alielekeza viongozi wa halmashauri, kata na vijiji kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria ndogo za usafi wa mazingira, huku akisisitiza kuchukuliwa hatua kwa watu wote watakaobainika kutupa taka hovyo katika maeneo ya umma.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Thecla Mkuchika, akiwahimiza wananchi wa kata ya Butiama kuzingatia usafi katika maeneo yao ya Biashara na makazi

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Butiama, Albinus Sasita, aliwataka wananchi kudumisha usafi katika maeneo ya biashara na makazi yao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kutokea ikiwemo kipindupindu .

Sauti ya Diwani wa Kata ya Butiama, Albinus Sasita akielezea umuhimu wa kila mwananchi kuzingatia hali ya usafi ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu
Diwani wa Kata ya Butiama, Albinus Sasita, akiwataka wananchi kudumisha usafi katika maeneo ya biashara na makazi yao. Picha na Absalom Tweve

Wananchi wa Butiama wamepokea kampeni hiyo kwa matumaini makubwa, wakiahidi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake. Kampeni ya “Ondoa Taka Butiama” inatarajiwa kufanyika kila Jumamosi kwa ushirikiano wa wananchi, viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa lengo la kuimarisha usafi wa mazingira na afya ya jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ni Bi. Aziza Baruti. akishiriki kwa vitendo kampeni ya “Ondoa Taka Butiama” iliyozinduliwa na mkuu wa wilaya ya Butiama, Thecla Mkuchika. Picha na Absalom Tweve