Butiama FM Radio

Butiama: waendesha Baiskeli 210 waenzi urithi wa Baba wa taifa

14 October 2026, 8:49 pm

Madaraka Nyerere ambae ni mtoto wa hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akimvisha medeli mmoja wa washiriki wa mashindano ya baiskeli kutoa Dar es salaam mpaka Butiama mkoani Mara. picha na Amos Marwa.

Waendesha baiskeli 210 wamewasili Butiama kuenzi miaka 27 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, wakihamasisha amani, umoja, uzalendo na maendeleo kupitia elimu, afya na utunzaji wa mazingira

Na Amos Marwa

Waendesha baiskeli 210 wamewasili wilayani Butiama, mkoani Mara, wakitokea safari ya zaidi ya kilomita 1,652 kwa lengo la kuenzi miaka 27 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza kuhusu safari hiyo, kiongozi wa msafara huo, Gabriel Landa, amesema wameadhimisha kumbukumbu hiyo kwa vitendo kwa kuendeleza amani, upendo, umoja na uzalendo, sambamba na falsafa ya Mwalimu Nyerere ya kupambana na ujinga, maradhi na umasikini, kwa kugawa madawati zaidi ya 5,000, kupanda miti zaidi ya 200,000 na kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ili kuboresha afya.

Sauti ya kiongozi wa msafara ,Gabriel Landa,

Kwa upande wake, Hillary Njau kwa niaba ya waendesha baiskeli wenzake amewaomba wadhamini kuendelea kuunga mkono mashindano hayo kutokana na manufaa yake.

Sauti Hillary Njau kwa niaba ya waendesha baiskeli wenzake.

Waendesha Baiskeli wakiwasili wilaya ya Butiama mkoa wa mara wakitokea Dar es salaamu katika maadhimisho ya Nyerere day. picha na Amos Marwa.

Wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo wamewataka Watanzania kuendelea kuenzi mema yaliyoachwa na Mwalimu Nyerere, hususan umoja, mshikamano, upendo na uzalendo.

Sauti za wananchi waliohudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 27 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Maelfu ya wananchi wa wilaya ya Butiama na nje ya Butiama waliojitokeza katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 27 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. picha na Amos Marwa

Maadhimisho hayo yameendelea kuwa chachu ya kuhamasisha jamii kudumisha tunu za Taifa na kuendeleza juhudi za kupambana na changamoto za maendeleo kwa vitendo, kama alivyosisitiza Baba wa Taifa.