Butiama FM Radio

Waziri Mkuu: Msipuuze tahadhari ya el niño

3 October 2026, 7:58 am

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. picha na Amos Marwa

“Tumetahadharishwa kuwa huenda kutakuwa na mvua kubwa za El Niño na sehemu zilizotajwa ni sehemu hii ya Kanda ya Ziwa. Niwaombe ndugu zangu wana Mwibara, ndugu zangu wana Mara, tusipuuze tahadhari hii.” Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba

Na Amos Marwa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wananchi wa Mkoa wa Mara, hususan wanaoishi katika maeneo hatarishi, kutopuuza tahadhari zinazotolewa kuhusu uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa za El Niño na kuchukua hatua za mapema kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza.

Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili mkoani Mara, Amesema maandalizi ya mapema ni muhimu kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua hizo.

Sauti ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mwibara Kangi Alphaxard Lugola, alipowasili katika jimbo hilo. Picha na Amos Marwa

Waziri Mkuu pia amewataka wataalamu na mamlaka zinazohusika kuendelea kufanya marekebisho na maandalizi katika maeneo yanayohitaji hatua za haraka, ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa na mamlaka.

Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. picha na Amos Marwa