Butiama FM Radio
Butiama FM Radio
22 October 2026, 12:52 pm

Kutokana na mwingiliano wa watu kati ya Tanzania na Kenya, wananchi wa Wilaya ya Butiama wameiomba Serikali kuongeza elimu kwa jamii kuhusu Ebola na namna ya kujikinga na ugonjwa huo
Na Amos Marwa
Wananchi wa Wilaya ya Butiama wameiomba Serikali kuongeza elimu kwa jamii kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ili kuwajengea uelewa wananchi kuhusu ugonjwa huo na namna ya kujikinga, wakieleza kuwa wengi wao wamepata taarifa kupitia vyombo vya habari pekee.
Wakizungumza na Butiama FM kwa nyakati tofauti, wamesema elimu hiyo inapaswa kutolewa kupitia mikutano ya hadhara na makongamano yatakayowashirikisha wananchi moja kwa moja, ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Mara unapakana na Kenya, ambako kumeripotiwa visa tisa vya ugonjwa huo.
Kwa upande wake, Wizara ya Afya imesema hadi sasa hakuna kisa cha Ebola kilichoripotiwa nchini, huku ikiendelea kuchukua hatua za tahadhari kuzuia uwezekano wa kuingia na kuenea kwa ugonjwa huo.