Soko la Mbuyuni lateketea kwa moto
6 February 2024, 8:26 am
Soko la Mbuyuni limeteketea kwa moto na kuwasababisha hasara kwa wafanyabiashara wa soko hilo huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.
Na Elizabeth Mafie
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amefika soko la Mbuyuni lililoteketea kwa moto usiku huu na kutoa pole na maagizo .
Akiambatana na kamati ya ulinzi Wilaya na Mkoa RC Babu amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya uchunguzi vinachunguza tukio hilo la moto.
Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa hakuna kilicho bakia na kwamba anawapa pole wafanyabiashara na kuwataka wawe watulivu wakati tukio hilo likichunguzwa ili kubaini chanzo cha moto huo.
Aidha amekemea tabia ya baadhi ya watu kutumia matukio kama hayo kufanya uporaji kwani haipendizi na badala yake wajikite katika kutoa msaada zaidi.
Nao wafanyabiashara wa soko hilo wamesema kuwa wamepata hasara kwani moto huo umeteketeza mali zao na kwamba wanaiomba serikali kushughulikia swala hilo.
Moto huo ulianza soko la Mbuyuni katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro majira ya saa saba usiku ambapo chanzo cha cha moto huo bado hakijajulikana.