Highlands FM

Wakulima wa pareto mkoa mbeya na songwe watakiwa kuzingatia ubora wa uzalishaji wa zao hilo.

31 May 2024, 17:19

Wafanyakazi wa kampuni ya Pareto {PCT} Wakiongozwa na Afisa wa Pareto Mkoa wa Mbeya na Songwe Mussa Malubalo.

Pareto ni  moja kati ya zao la kibiashara ambalo hulimwa mikoa sita tu nchini tanzania, zao hilo ni jamii ya maua hutumika kutengenezea dawa za kuuwa wadudu.

Na Lameck Charles

Highlands Fm Radio

Serikali ya Wilaya ya Mbeya imesema itaendelea kuhakikisha zao la pareto linakuwa bora kwa kuhakikisha wanunuzi wanafuata utaratibu uliopo ili kuepuka na  hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya vishoka wa zao hilo.

Rai hiyo imetolea na Mkuu wa Wilaya  ya Mbeya Beno Malisa wakati akizungumza na wanunuzi wa makampuni ya pareto wa mikoa ya Mbeya na Songwe.

Sauti Benno Malisa
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Benno Malisa akizungumza na wanunuzi wa Pareto

Aidha Beno Malisa amesema wilaya ya Mbeya ina kampuni tisa za ununuzi wa zao hilo la kibiashara na kuzitaka kampuni hizo kuwajibika kwa kulipa kodi za halmashauri kwa lengo la kuleta maendeleo ya halmshauri husika.

Sauti Malisa

Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa makapuni ya ununuzi wa pareto  ikiwemo kampuni ya PCT wamesema msimu uliomalizika walipata hasara kutokana na ununzi wa maua yasiyokidhi viwango hivyo ni  matumaini yao misimu ujao wa mavuno watanunua maua yaliyo bora ikiwa ni kuwaelimisha wakulima na mawakala wao.

Sauti Wawakilishi
Wanunuzi wa zao la Pareto Mbeya na Songwe

Lucas Ayo ni Mkurugenzi wa  wa Zao la pareto Tanzania amewasihi wanunuzi wa zao la pareto kushikamana na kuwa pamoja  kwa utekelezaji waliyokubaliana ikiwemo kuto nunua maua yasiyo kauka.

Sauti Mkurugenzi

Kikao hicho kilichokaliwa kwa lengo la kufanya tathmini ya zao la Pareto huku hali ya uzalishaji wa zao hilo ikipanda kutoka tani elfu mbili hadi kufikia tani elfu nne kwa sasa.