‘Jizingatie’ kuwanusuru vijana na maambukizi ya Ukimwi
16 December 2023, 16:26
Na Prince Fungo
Mwandishi wa Habari
Highlands Fm radio
Tanzania inaweza kufikia lengo la kuondokana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi ifikapo mwaka 2030 ikiwa wananchi watatambua umuhimu wa kupima afya zao.
Pia wamesisitizwa ili kufikia lengo hilo la kimkakati ni lazima wachukue taadhari ikiwemo kuepuka ngono zembe.
Hayo yamejiri wakati shirika lisilokuwa la kiserikali HJMRI kwa kushirikiana na taasisi ya afya ckeck wakizindua mpango wa jizingatie ambao umelenga kuhamasisha wananchi hasa vijana wenye umri kuanzia 15 hadi 24 kupima na kujilinda.
Akitoa maelezo wakati wa zoezi hilo kwenye viwanja vya Luanda nzovwe jijini Mbeya mratibu wa kambi za afya check Dr. Isaac Maro Amesema kuna umuhimu wa wananchi kupima afya zao ili kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ukimwi.