

6 March 2025, 5:32 pm
Utaratibu wa kupima afya kwa mkulima utamsaidia kujua mapema endapo amepata maambukizi ya magonjwa kipindi cha kilimo
Na Nyamizi Mdaki
Wakulima Wilayani Uyui mkoani Tabora wametakiwa kuwa na utaratibu wa kupima afya mara baada ya msimu wa kilimo kumalizika ili kulinda afya zao.
Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza wilaya ya Uyui Daktari Joseph Werema amesema kupima afya kutamhakikishia usalama wake kwasababu huenda akawa amepata maradhi kipindi cha shughuli za kilimo.
Naye, Mkulima wa Imalamihayo Abdallah Masua anasema kwamba hazingatii kanuni bora za kilimo kwasababu hajapata elimu hiyo.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Wilaya ya Uyui Bahati Fundi anaeleza madhara ambayo mkulima anaweza kuyapata asipozingatia kanuni bora za kilimo.
Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza wilaya ya Uyui Daktari Joseph Werema amesema kwamba Kilimo na Afya ni pande mbili za sarafu,hivyo wanatambua na kuthamini mchango wa wakulima.