Uyui FM Radio

Wanahabari kuwa mabalozi kutoa elimu ya sikoseli

11 September 2023, 3:17 pm

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya kujenga uelewa wa sikoseli

Mkoa wa Tabora unashika nafasi ya nne miongoni mwa mikoa yenye waathirika wengi wa ugonjwa wa sikoseli nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa hospital ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete Dkt. Renatus Burashahu amewaomba waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa jamii ili kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo sikoseli kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Dkt. Burashahu amesema hayo wakati wa mafunzo mafupi kwa waandishi wa habari mkoani Tabora yenye lengo la kujenga uelewa juu ya ugonjwa huo.

Kaimu mkurugenzi Renatus Burashahu

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto Hospitali ya Rufaa Kitete Amon Rrakitimbo amesema licha ya kuhisi maumivu makali ya mara kwa mara ni rahisi kwa wagonjwa wa sikoseli kupata maambukizi ya magonjwa mengine.

Sauti ya Daktari Amon

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaungana na dunia kuadhimisha mwezi wa kujenga uelewa kwa jamii juu ya ugonjwa wa sikoseli ambapo maadhimisho hayo yameanza septemba 5 hadi 30 mwaka huu.