

25 March 2021, 4:14 pm
Wafanyabiashara na wajasiriamali katika Manispaa ya Tabora wamesema watamkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt John Pombe Magufuli kutokana na namna alivyo wapigania na kupata maeneo ya kufanyia biashara bila Bugudha.
Wafanyabiashara hao akiwemo Haki Kasawa,Sheila Chambuso na Muniru Butala wamesema Rais Magufuli mbali na kuwatetea wanyonge alihakikisha wafanya biashara pia wanajitegemea na kupata faida katika biashara zao ili kuendeleza Tanzania ya viwanda.