Uyui FM Radio

Mufti ahimiza waislam kushirikiana na serikali

7 October 2021, 7:53 pm

Mufti Mkuu wa Tanzania sheikh Abubakar Zubeir Ally amewataka viongozi wa dini ya kiislam mkoani Tabora kuendeleza ushirikiano na viongozi wa serikali ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi, weledi pamoja  na kuzingatia madili ya dini.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar

Wito huo ameutoa mjini Tabora wakati akizungumza na viongozi wa dini, serikali pamoja na waumini wa dini ya kiislam kwenye ukumbi wa isike Mwana kiyungi  kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.

Sauti ya Mufti

Awali mkuu wa mkoa wa Tabora Dokta Batilda Buriani amemkaribisha Mufti mkuu wa Tanzania mkoani Tabora huku akisema kuwa mkoa bado unafursa nyingi hivyo  katika miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Reli ya kisasa na Bomba la mafuta ghafi.

RC Tabora
Sauti ya RC Tabora

Naye Sheikh wa mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amesema kuwa Ujio wa Mufti ni njia moja wapo ya kuendelea kufahamu miradi mbalimbali ya kiuchumi na  kijamii iliyopo kwa manufaa mkoa na taifa kwa ujumla.