Uyui FM Radio

RC Chacha awataka watumishi kuwatendea haki wananchi

19 March 2024, 4:20 pm

Baadhi ya watumishi wa mkoa wa Tabora.Picha na Mohamed Habibu

watumishi mkoani Tabora wametakiwa kufanya kazi kwa bidii huku wakiwatendea haki wananchi.

Na Zaituni Juma

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amewataka watumishi mkoani hapa kuuthamini umma wanao uongoza.

Ametoa rai hiyo mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiwa ni sehemu ya mapokezi yaliondaliwa na watumishi wa ofisi yake.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Chacha akizungumza na watumishi.Picha na Mohamed Habibu
sauti ya mkuu wa mkoa

Akizungumza kwa niaba ya vyombo vya usalama kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokozi mkoa wa Tabora SACF Mohamed Shauri amesema jamii ina matarajio makubwa na kiongozi huyo mpya wa mkoa.

Sauti ya SACF Mohamed Shauri

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Igalula Venant Daud amesema wabunge wa Tabora watampatia ushirikiano katika Nyanja mbalimbali.

Sauti ya Mbunge Venant

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhan Kapela amesema kwamba Serikali inauangalia mkoa wa Tabora kwa jicho zuri na kufikia hatua ya kuwapandisha hadhi watumishi wengi waliokuwa ngazi za chini.