Uyui FM Radio

DC Mwansasu: Mkizidiwa vaeni kondomu

15 April 2024, 10:52 pm

Baaadhi ya wavuvi wa kata ya Loya wilayani Uyui.Picha na Elisha Lusatila

Vijana ni nguvu kazi ya taifa kwahiyo lindeni afya zenu na mhakikishe mnacheza kwa uangalifu

Na Elisha Lusatila

Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Zakaria Mwansasu amewasihi wananchi kulinda afya zao dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Mwansasu ametoa rai hiyo kwenye ziara yake ya kikazi akiwa katika kata ya Loya, akisema kwamba ni vyema watu wakazingatia matumizi ya kinga.

Mkuu wa wilaya Mwansasu akizungumza na wavuvi wa Loya.Picha na Elisha Lusatila
Sauti ya Dc Mwansasu

Vile vile kiongozi huyo amepiga marufuku watoto kuwaacha kwenye makambi ya uvuvi kwakuwa ni hatari kwao.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Zakaria Mwansasu

Mkuu huyo wa wilaya ya Uyui Zakaria Mwansasu amesema kwamba UKIMWI bado upo na unaua. hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini kujilinda.