Uyui FM Radio

Asilimia 90 kesi zinazoripotiwa mahakama ya wilaya Uyui ni za ubakaji

31 January 2024, 1:29 pm

Hakimu mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Tausi Mongi akiwa na Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo Upuge Jackline Lukuba katika studio za 99.3

Asilimia 90 ya kesi zinazoripotiwa katika mahakama ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora ni za ubakaji.

Na Zaituni Juma

Hakimu mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora Tausi Mongi amesema asilimia 90 ya kesi zinazoripotiwa katika mahakama hiyo ni za ubakaji.

Akizungumza kwenye kipindi cha Kifungua Kinywa, Mongi amesema kwamba kesi hizo husababishwa na uelewa mdogo wa masuala ya sheria.

Sauti ya hakimu Tausi Mongi

Kwa upande wake Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo Upuge wilayani Uyui Jackline Lukuba amewasihi wananchi kuhudhuria viwanja vya mahakama ya wilaya pamoja na zile za mwanzo kupata elimu bure ya sheria.

Sauti ya Jackline Lukuba

Kauli mbiu ya wiki ya sheria mwaka 2024 ni umuhimu wa zana ya haki kwa ustawi wa Taifa, nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai.