Uyui FM Radio

Wananchi Tabora waaswa kumuenzi Wakasuvi kwa uchapakazi

13 April 2024, 6:51 pm

Rc Chacha akiwa na baadhi ya viongozi kwenye kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora.Picha na Mohamed Habibu

Marehemu Wakasuvi alikuwa mchapakazi lakini pia alikuwa na mahusiano mazuri na watu hivyo dumisheni amani na ushirikiano.

Na Zaituni Juma

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amewataka wananchi kuendelea kuyaenzi yale aliyokuwa akiyatenda aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Marehemu Hassan Wakasuvi enzi za uhai wake.
Ametoa rai hiyo alipofika nyumbani kwa marehemu kata ya Mabama wilayani Uyui kwa ajili ya kuisalimia familia.

Rc Chacha akiwa na mke wa marehemu Wakasuvi pamoja na watoto wake.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya mkuu wa mkoa Chacha

Kwa upande wake diwani viti Maalum kata ya Mabama ambaye ni mmoja wa watoto wa marehemu Wakasuvi, Amina Wakasuvi amewashukuru wanatabora na watanzania kwa kuwapa faraja.

Sauti ya Amina Wakasuvi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa Hassan Wakasuvi alifariki dunia tarehe 22 Februari, 2024.