Uyui FM Radio

21 mbaroni wizi miundombinu ya maji

4 July 2023, 11:07 am

Kamanda Richard Abwao akionesha baadhi ya vifaa vilivyokamatwa.Picha na Mohammed Habibu

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu 21 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo mbali mbali vya uhalifu vikiwemo vya wizi wa vifaa vya miundo mbinu ya maji.

Na Nicholaus Mwaibale

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi Richard Abwao amesema Watuhumiwa hao wamekamatwa katika misako mbali mbali inayofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na Wananchi

Baadhi ya vifaa vilivyokamatwa na jeshi la polisi.Picha na Mohammed Habibu

Jeshi la Polisi linaendelea na oparesheni mbali mbali za kuwasaka Wahalifu

Jeshi la Polisi linaendelea na oparesheni mbali mbali za kuwasaka Wahalifu na wanaojihusisha na wizi wa miundo mbinu ya idara ya maji na linawaomba wananchi mkoani Tabora kutoa taarifa za Watu wanaofanya vitendo hivyo

Sauti ya Kamanda Richard Abwao

Katika tukio lingine Kamanda Abwao amesema mtu mmoja mkazi wa Usule Benedicto Mangi ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo.

Sauti ya Kamanda Richard Abwao