Uyui FM Radio

Zaidi ya wasichana 200,000 kufikiwa na chanjo ya HPV Tabora

23 April 2024, 7:10 pm

Baadhi ya wanafunzi na viongozi waliohudhuria uzinduzi wa chanjo.Picha na Mohamed Habibu

Kampeni ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 imezinduliwa nchini naitafanyika kwa siku 5 mfululizo.

Na Mohamed Habibu

Wazazi na walezi  wenye  wasichana walio na  umri wa miaka 9 hadi 14 mkoani Tabora  wametakiwa kuwaruhusu  kupata chanjo ya kuzuia  saratani ya mlango wa kizazi  ili kuwaepusha  na maambukizi ya ugonjwa huo.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Paulo chacha amesema hayo wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo uliofanyika  shule ya msingi kizigo iliyopo Manispaa ya Tabora.

Mkuu wa mkoa Paul Chacha akizungumza kwenye uzinduzi wa chanjo.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya mkuu wa mkoa

Kwa upande wake Afisa elimu Mkoa wa Tabora JUMA KAPONDA amesema kuwa walimu mkoani  hapa wako tayari kuwapa ushirikiano wataalam wa afya huku akiwasisitiza wazazi kuiamini serikali.

Afisa elimu Mkoa wa Tabora JUMA KAPONDA.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Afisa elimu

Hata hivyo mkuu wa mkoa Paul Chacha amezitaka Taasisi binafsi pamoja na umma kushirikiana kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa afya.