Uyui FM Radio

Migange aitupia lawama Mashujaa FC

14 July 2023, 11:10 am

Kocha Abdul Migange akiwa katika benchi la ufundi

Aliyekuwa kocha wa klabu ya mpira wa miguu ya Mashujaa FC Meja Mstaafu Abdul Migange amelaumu uongozi wa timu hiyo kutokana na kitendo cha kumuacha baada ya kuipandisha Ligi kuu ya Tanzania Bara

Na Mussa Nkoningo

Kocha aliyeipandisha timu Ya Mashujaa Fc Ligi kuu Meja Mstaafu Abdul Migange amesema uongozi wa klabu hiyo umeonesha dharau kwa kumuacha kwa sababu bado anauwezo mkubwa wa kufundisha timu ya ligi kuu.

Mashujaa FC imemtangaza Mohamed Abdallah Bares Kuwa kocha mpya

Migange amesema kuishusha timu ya ligi kuu kama Mbeya City kwa kuifunga michezo ya nyumbani na ugenini siyo jambo la fedha bali ni mipango ya mwalimu aliyoiandaa kuanzia mazoezini na kutekelezwa ndani ya uwanja.

Sauti ya Meja Mstaafu Abdul Migange

Mingange ameongeza kuwa viongozi wanatakiwa kuheshimu mchango wa makocha kabla na baada ya timu  kupata mafanikio.

Sauti ya Meja Mstaafu Abdul Migange

Aidha  Mashujaa FC imemtangaza Mohamed Abdallah Bares Kuwa kocha mpya na sasa inaendelea na utambulisho wa wachezaji wapya ambapo hadi sasa imemtangaza Adam Adam, Michael Masinda, Abdulnasir Asaa moh’d, pamoja na Nassor kiziwa kama wachezaji wapya.