Uyui FM Radio

Madiwani watakiwa kupambania chakula shuleni

18 August 2023, 5:27 pm

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza.Picha na Salma Abdul

Madiwani wamesisitizwa kuhakikisha upatikanaji wa chakula shuleni unazingatiwa.

Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo amewataka madiwani kushirikiana na walimu kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni ili wanafunzi wapate muda wa kutosha wa kujifunza.

Amesema hayo akiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani lililofanyika wilayani humo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Igunga
Dc Sauda Mtondoo akizungumza na madiwani.Picha na Salma Abdul

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Igunga akiwemo diwani viti maalum Eva Godfrey na  Diwani wa kata ya Bukoko Jidashema Mwandu wamesema watakwenda kusimamia suala hilo kwa kutoa elimu zaidi kwa wazazi na walezi juu ya umuhimu wa kuchangia chakula shuleni kwa ajili ya watoto wao.

Sauti za madiwani

Mkuu wa wilaya ya Igunga amesema Serikali ina lengo la kuhakikisha madarasa yote ya mitihani ya taifa wana pata chakula shuleni ili kuwapa nafasi nzuri zaidi wanafunzi kubaki shuleni kujifunza zaidi na hivyo kuongeza ufaulu kwenye masomo yao.