Uyui FM Radio

Malalamiko 62 yapokelewa TAKUKURU Tabora

18 April 2024, 4:20 pm

Mhandisi Abnery Mganga akizungumza na wanahabari.Picha na Omary Khamis

TAKUKURU imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusiana na vitendo vya rushwa na mengine kuhakikisha yanapelekwa kwenye mamlaka husika

Na Omary Khamis

Jumla ya malalamiko 62 yamepokelewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Tabora katika kipindi cha mwezi January hadi Machi mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora Mhandisi Abnery Mganga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uwasilishaji wa utekelezaji wa TAKUKURU ndani ya miezi mitatu.

Sauti ya Mhandisi Mganga

Katika hatua nyingine Mhandisi Mganga amewaomba wananchi na wadau wote kwa ujumla kuendelea kuunga mkono kwa kuzuia vitedo vya rushwa.