Uyui FM Radio

Baiskeli 58 zatolewa kwa vikundi vya wanawake UWT Tabora

13 July 2023, 11:49 am

Mbunge viti Maalum Munde akiwa kwenye mkutano soko kuu Tabora mjini na kugawa baiskeli kwa viongozi wa UWT. Picha na Mohamed Habibu

Jumla ya baiskeli 58 zimetolewa na kugawiwa; baiskeli mbili kila kata kwa vikundi vya wanawake UWT pamoja na vijana mkoani Tabora  ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Na Zaituni Juma

Mbunge wa viti maalum mkoani Tabora Munde Tambwe amesema baiskeli hizo zilizotolewa zina jumla ya thamani ya shilingi  laki mbili na elfu ishirini kwa kila baiskeli moja.

Sauti ya Munde Tambwe

Awali mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora Mwanne Mchemba amesema anahakika kwamba kupitia baiskeli hizo zilizotolewa kwa wanawake zitasaidia umoja huo kuwa imara kimaendeleo.

Sauti ya Mwanne Mchemba
Mwenyekiti UWT Mkoa wa Tabora Mwanne Mchemba akizungumza kwenye mkutano huo.Picha na Mohamed Habibu

Jumla ya baiskeli 58 zimetolewa na kugawiwa baiskeli mbili kila kata kwa vikundi vya wanawake UWT pamoja na vijana Mkoani Tabora  ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi, Hata hivyo Mbunge wa viti maalumu MUNDE amewasisitiza wanawake hao kuzitumia baiskeli hizo kwa manufaa ikiwemo kuongeza kipato.