Uyui FM Radio

Wawili mbaroni tuhuma kifo cha mwanafunzi wa chuo

14 August 2023, 4:32 pm

Kamanda Richard Abwao akizungumza na wanahabari.Picha na Samweli Ayub

Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa chuo cha Tabora polytechic ambae alipotea kwa takribani siku kumi.

Na Salma Abdul

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji cha tumbi Manispaa ya TABORA.

Sauti ya Kamanda wa Polisi

Kamanda ABWAO amesema hadi sasa watuhumiwa wawili ambao ni waendesha chombo cha usafiri aina ya pikipiki maarufu kama bodaboda wamekamatwa kwaajili ya mahojiano.

Sauti ya kamanda Richard Abwao

Hata hivyo kamanda ABWAO amesema uchunguzi utakapomilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.