

12 December 2021, 7:46 pm
Wanawake wamehimizwa kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa ni wahanga wakuu wa athari za mabadiliko ya tabia nchi katika jamii
Katibu mtendaji wa taasisi ya OHIDE Silesi Mali Mali amesema wanawake wamekuwa nguzo katika uendeshaji wa familia na wengi hutegemea kilimo na ujasiriamali hivyo mabadiliko ya tabia nchi huathiri shughuli zao moja kwa moja
Beatrice Venance kutoka shirika la Good Harvest ametoa wito kwa wanawake na jamii kwa ujumla kuendelea kutunza mazingira pamoja na kuendelea kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Wakati huohuo mkurugenzi wa shirika la Good Harvest Filbert Chundu amesema wanaendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kuanzia mashuleni na kupitia michezo ambayo inaambatana na upandaji miti
INSERT: FILBERT CHUNDU
Hayo yanajili wakati ambapo Tanzania na nchi nyingi duniani zikikabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaathiri upatikanaji wa mvua,shughuli za kilimo na uzalishaji hali inayotishia ukosefu wa chakula na kudolola kwa uchumi duniani