Uyui FM Radio

Safari ya mwisho ya mtangazaji Beatrice Mahangi

10 February 2023, 1:52 pm

Ibada ya mazishi ya  mtangazaji wa kipindi cha BEMBEA LA WATOTO  BEATRICE JOSEPH MAHANGI  wa  kituo cha redio UFR 99.3 Tabora imefanyika   hii leo februari 10 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Paul-Bunda mkoani Mara.

Viongozi wa UFR wakiungiza mwili Kanisani

Awali Meneja wa kituo  cha redio UFR  Nicolaus Mwaibale amesema  enzi za uhai  wa mfanyakazi wa kituo hicho  Betriece  JOSEPH alikuwa ni mchapakazi na muadilifu.

sauti ya meneja Mwaibale

Nao baadhi ya wafanyakazi wenzake  wamesema kuwa hawatomsahau Bietriece kwa ucheshi wake na kuwapenda watu wote.

wafanyakazi,ndugu na jamaa wakiaga mwili
sauti za wafanyakazi Ufr

Mtangazaji Beatrice Joseph Mahangi alifariki mnamo februari 7,2023  wilayani Bunda ambako alikuwa akipatiwa matibabu,Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.