Uyui FM Radio

Zaidi ya bilioni moja kujenga shule za msingi Tabora

3 July 2023, 12:22 pm

Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Mabatini iliyopo kata ya Tambukareli Tabora Manispaa.Picha na Mohammed Habib

Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 1 na milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za msingi kwenye kata za Mtendeni, Mbugani na Tambukareli manispaa ya Tabora ili kuondoa tatizo la upungufu wa madarasa katika manispaa hiyo.

Na Zaitun Juma

Hayo yamebainishwa na mstahiki meya manispaa ya Tabora Ramdhani Kapela ambaye amesema mbali na kuboresha miundombinu ya elimu pia miradi hiyo inachochea maendeleo kwenye kata husika kupitia ajira.

Sauti ya Ramadhani Kapela

Akizungumzia ujenzi wa shule mpya ya msingi Mabatini, afisa mtendaji kata ya Tambukareli Hussein Majimoto amesema kwa sasa upo katika hatua ya upauaji.

Sauti ya Hussein Majimoto

Kwa mujibu wa afisa mtendaji Majimoto amesema ujenzi wa shule mpya ya msingi Mabatini ambao umejumuisha madarasa 7,ofisi moja na shule ya awali ya mfano utaondoa changamoto ya upungufu wa madarasa uliopo.