

27 January 2025, 2:42 pm
Picha ikiwaonyesha wadau mbalimbali wa mahakama wakiwa katika jengo la NSSF mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amewataka wadau wa mahakama kushirikiana kutimiza malengo ya maadhimisho ya wiki ya sheria.
Ametoa wito huo leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria iliyofanyika katika viwanja vya NSSF karibu na TBC Tabora.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Poul Chacha
Kaimu Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Tabora Daktari Mwajuma Kadilu amewasihi wananchi kujitokeza kwenye viwanja hivyo kupata elimu zaidi.
Sauti ya kaimu jaji mfawidhi Daktari Mwajuma Kadili
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka 2025 nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo.