

7 July 2024, 7:18 pm
Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kitaifa yamefanyika mara ya nne mfululizo mkoani Tabora yakibeba kaulimbiu isemayo “Ushirika hujenga kesho iliyo bora”
Na Nicholaus Mwaibale
Naibu Waziri Mkuu na waziri wa nishati Daktari Dotto Biteko amewataka viongozi wa ushirika nchini kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya watanzania masikini ili kuwaisaidia kukuza uchumi.
Daktari Biteko ametoa maagizo hayo wakati wa kufunga maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani kitaifa ambayo yamefanyika katika viwanja vya nanenane Ipuli ,Manispaa ya Tabora.
Naye Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema msimu huu Sekta ya Tumbaku imezalisha wastani wa tani laki moja ukilinganisha na mwaka jana ambapo zilizalishwa tani elfu 60 tu, huku akibainisha changamoto walizokumbana nazo wakulima katika kipindi hiki cha uzalishaji wa tumbaku.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amesema kuwa masoko ya tumbaku na pamba yanaendelea vizuri na wananchi wanaendelea na masoko bila manunguniko.