Uyui FM Radio

Milioni 561 za punguza msongamano madarasani

6 May 2024, 1:03 pm

Baadhi ya madarasa katika shule mpya ya msingi Kidatu.Picha na Mohamed Habibu

Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa ya Tabora ilipokea bilioni 1.8 kupitia mradi wa boost kwaajili ya kujenga shule mpya 3 na zingine kukarabatiwa.

Na Mohamed HabibuJumla ya shilingi milioni 561 zimetumika kujenga shule ya msingi KIDATU Manispaa ya Tabora ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Magereza.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora ELIAS KAYANDABILA amesema, hayo wakati wa ziara yake shuleni hapo kwa lengo la kufuatilia ufundishaji na maendeleo ya wanafunzi kwa ujumla.

Mkurugenzi Elias Kayandabila akizungumza na waandishi wa habari.Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Elias Kayandabila

Kwaupande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kidatu IMANI SANKE amesema shule hiyo ina vyumba vya madarasa 14,matndu ya vyoo 18 pamoja na jengo la elimu ya awali lenye vyumba viwili vya madarasa.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kidatu IMANI SANKEY..Picha na Mohamed Habibu
Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kidatu, Imani Sanke

Nao baadhi ya wazazi NEEMA CHAKOKO na HAMZA JUMA wameipongeza serikali kwa kukamilisha mradi huo kutokana na changamoto za awali ikiwemo ikiwemo wanafunzi kutembea umbali mrefu na msongamano mkubwa madarasani.

Baadhi ya wazazi wenye watoto shuleni hapo.Picha na Mohamed Habibu
Sauti za wazazi Neema Chakoko na Hamza Juma