Wananchi milioni 1.6 wapatiwa chanjo ya UVICO 19 Tabora.
5 May 2024, 3:34 pm
Na Zaituni Juma
Serikali mkoani Tabora imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la CARITAS Tabora katika utoaji wa chanjo ya UVICO 19 ili kumfikia kila mwananchi.Na
Zaidi ya watu milioni 1,600,000 wamepatiwa chanjo ya UVICO 19 kwa mkoa wa Tabora tangu kuanza kutolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni sawa na asilimia 112.
Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Daktari Honorata Rutatinisibwa amesema hayo katika ukumbi wa JM Hoteli wakati wa kuhitimisha mradi wa utoaji wa chanjo ya UVICO 19 kwa kipindi cha mwaka 2023 ulioratibiwa na shirika la Cartas Tabora.
Naye mkurugenzi wa shirika la CARTAS TABORA Padri Paschal Kitambi amesema wataendelea kutekeleza miradi mbalimbali ili kuigusa jamii moja kwa moja.
Kwa upande wake, Daktari wa shirika hilo MARIAMU MIKINDA amesema katika kutekeleza mradi wa utoaji wa chanjo ya UVICO 19 kwa kipindi cha mwaka mmoja wamefikia vituo vya afya 65 na kutoa chanjo kwa watu elfu 43 kwa wilaya za Kaliua na Uyui.