

6 March 2025, 4:43 pm
wahitimu wameaswa kuzingatia waliyofundishwa na walimu wao.
Na Nicolaus Mwaibale
Diwani wa kata ya Ndono katika halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Mrisho Ally ameahidi kuzifikisha kwenye baraza la madiwani changamoto za shule ya Sekondari Ndono.
Ametoa ahadi hiyo alipomwakilisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui Lubasha Makoba kwenye mahafali ya kidato cha 6 yaliyofanyika shuleni hapo.
Katika mahafali hayo Afisa elimu wa kata ya Ndono Kristina William na mwenyekiti wa jumuia ya wazazi katani hapo Yahaya Maulidi wametoa ushauri kwa wazazi pamoja na wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha 6 mwaka huu.
Kwa upande wao wazazi Issa Ruje na Tabia Mohamedi wameeleza namna walivyo upokea ushauri uliotolewa na mgeni rasmi na kuwasihi wazazi wengine kuuzingatia.
Hayo ni mahafali ya nane ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Ndono yenye jumla ya wanafunzi 1,759 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha Sita.