Uyui FM Radio
Asilimia 68 ya wanafunzi wameandikishwa darasa la kwanza Manispaa ya Tabora.
14 January 2025, 6:01 pm
Na, Nyamizi Mdaki
Asilimia 68 ya wanafunzi wameandikishwa darasa la kwanza, kwenye Shule mbalimbali za Serikali katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
Hayo yamebainishwa na Afisa elimu awali na msingi Manispaa ya Tabora Patricia Mbigili wakati akizungumza na UFR kuhusu hali ya uandikishaji.
Aidha ameongeza kuwa ifikapo Machi 31 kwa mzazi ambaye atakuwa hajamwandikisha mtoto wake atachukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kupelekwa kwenye mabaraza ya kata, vituo vya polisi na hata mahakamani.
Shule zote nchini zimefunguliwa January,13 2025 huku serikali ikitarajia kuona asilimia kubwa ya wanafuzi wakianza shule kutokana na elimu kutolewa bure kuanzia awali hadi kidato cha sita